Kitabu hiki ni toleo la pili katika msururu wa Shujaa Wangu ni Wewe, lililoandaliwa na Kikundi cha Rufaa cha Kamati ya Kudumu ya Mashirika
Mbalimbali kuhusu Afya ya Kiakili na Msaada wa Kisaikolojia katika Mazingira ya Dharura (IASC MHPSS RG). Mradi huu ulisaidiwa na
wataalamu kutoka ulimwenguni, maeneo na wa kitaifa kutoka Mashirika Wanachama wa IASC MHPSS RG, pamoja na wazazi, walezi, walimu
na watoto kutoka kote ulimwenguni.
Mwanzoni mwa janga la COVID-19, zaidi ya watoto 1700 kutoka nchi 104 walisaidia kubuni kitabu cha hadithi cha watoto kuhusu COVID-19
kilichowafikia mamia ya maelfu ya watoto kote ulimwenguni. Hadithi hii ilikuwa kisa cha mafanikio sana ulimwenguni kote katika kuwafikia
watoto, ikiwa na zaidi ya tafsiri 140 na orodha kubwa ya marekebisho ya picha. Leo hii, watoto wengi bado wanaishi na mabadiliko katika
mazoea yao ya kila siku kwa sababu ya janga hili na wanakabiliana na masuala yanayoathiri ustawi wao wa kiakili. Matatizo mengi yaliyoko
kwa sasa sio sawa na jinsi yalivyokuwa mwanzoni mwa janga hili.